MBUNGE WA KIMILILI AANDIKISHA TAARIFA BAADA YA KUVAMIWA NA MKAZI.
Mbunge wa Kimilili katika kaunti ya Bungoma Didmus Baraza ameandikisha taarifa katika kituo cha polisi cha Kimilili kufuatia tukio ambapo alivamiwa na mkazi mmoja katika hafla ya mazishi na kumpokonya kipaza sauti.
Akizungumza baada ya kuandikisha taarifa hiyo jana, Baraza ametaka idara ya usalama kumchukilia hatua mkazi huyo ili kuwa mfano kwa wengine na kuzuia kutokea hali kama hiyo katika siku za usoni.
Wakati uo huo Baraza amelaumu vyombo vya usalama kwa kutokuwa makini katika kuhakikisha usalama unaimarishwa maeneo ambako kunaandaliwa hafla za mikusanyiko ya watu hali inayopelekea kushuhudiwa visa kama hivi.
Ni kisa ambacho pia kimekashifiwa vikali na baraza la wazee wa jamii ya bukusu katika kaunti hiyo ya Bungoma.