MBUNGE WA KACHELIBA MARK LUMNOKOL APIGIA DEBE CHAMA CHA UDA


Mbunge wa Kacheliba kaunti ya Pokot Magharibi Mark Lumnokol ameendelea kupigia debe chama cha UDA ambacho kinahusishwa na naibu rais William Ruto.
Lumnokol amekariri kauli ya Ruto kuwa UDA na ODM ndivyo vyama vyenye sura ya kitaifa huku akipuuzilia mbali muungano wa vyama vya ANC, Ford Kenya na Wiper anaosema umesheni vyama vya kikabila.
Wakati uo huo Lumnokol ameelezea imani kuwa Ruto atatwaa uongozi wa taifa baada ya uchaguzi mkuu ujao akisema ndiye kiongozi anayestahili kuliongoza taifa kutokana na mipango aliyo nayo kwa taifa hili.