MBUNGE SAMUEL MOROTO AITAKA SERIKALI YA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI KULIPA MADENI YOTE


Mbunge Wa Kapenguria Samuel Moroto Ameitaka Serikali Ya Kaunti Ya Pokot Magharibi Kuwalipa Watu Madeni Ambayo Yamekawia Kulipwa Kwa Zaidi Ya Mwaka Mmoja Sasa.
Moroto Amesema Baadhi Ya Wakazi Wanaendelea Kuhangaikia Maisha Yao Kwa Kushindwa Kulipa Mikopo Waliyoichukua Kwenye Benki.
Na Kuhusiana Na Masoko Ambayo Yamekawia Kufunguliwa Likiwamo La Mji Wa Makutano Moroto Amemtaka Gavana John Lonyangapuo Kuyafungua Ili Wanabiashara Wafaidike Kwenye Biashara Mjini Humo.
Moroto Aidha Ameendelea Kuikosoa Ripoti Ya Jopo La Upatanishi Bbi Huku Akisema Ripoti Hiyo Inalenga Kuwanufaisha Viongozi Wakuu Nchini Huku Mwananchi Wa Kawaida Akiendelea Kubebeshwa Mizigo Zaidi.