MBUNGE MARK LOMUNOKOL AMEITAKA SERIKALI KUCHUNGUZA MADAI YA KUKAMATWA NA KUULIWA KWA WATU SITA KATIKA ENEO LA CHEMOLINGOT KAUNTI YA BARINGO


Mbunge wa Kacheliba Mark Lomunokol ameitaka serikali kuchunguza madai ya kukamatwa na kuuliwa kwa watu sita katika eneo la Chemolingot kwenye kaunti ya Baringo, mauaji ambayo yanadaiwa kutekelezwa na maafisa wa polisi mwanzoni mwa mwezi huu.
Lomunokol amemtaka mwenyekiti katika Idara ya Usalama wa ndani kueleza zaidi kuhusu mauaji hayo pamoja na changamoto zinazowakumba maafisa wa upelelezi katika kuyatekeleza majukumu yao kikamilifu kuhusiana na visa hivyo vya kusikitisha.
Vilevile Lomunokol ameitaka serikali kutafuta suluhu ya kudumu kutokana na utovu wa usalama miongoni mwa wakazi wa Baringo huku akitaka pia wizara ya usalama wa ndani kuelezea mahali walipo watu wanne walioruhusiwa kuondoka kutoka kituo cha polisi cha Eldama Ravine na ambapo hawajarejea nyumbani hadi sasa.