MBITO ATAKIWA KUOMBA MSAMAHA KUHUSU MATAMSHI YAKE DHIDI YA MFANYIBISHARA TRANS NZOIA.


Seneta wa kaunti ya Trans nzoia Michael Mbito ametakiwa kuomba msamaha kwa kumwita mfanyibiashara Nathaniel Tum mnyakuzi mkuu katika mzozo wa umiliki wa kipande cha ardhi cha ekari 10 baina ya Tum na usimamizi wa Kitale school.
Baraza la wazee katika kaunti hiyo wakiongozwa na Paul Mengich na Darius Ngei wamesema kuwa watalazimika kufanya maandamano na kuwasilisha kesi mahakamani iwapo Mbito hatoomba msamaha.
Hata hivyo seneta mbito ameshikilia kuwa ni sharti vipande vyote vya ardhi ya umma vilivyonyakuliwa na bwenyenye huyo vitwaliwe na serikali ikiwemo mashamba ya kampuni ya kuzalisha mbegu Kenya seed.
Itakumbukwa kuwa tarehe 10 mwezi mei mwaka 2010 tume ya kitaifa ya ardhi ilifutilia mbali hati miliki ya kipande hicho cha ardhi kabla ya ripoti ya ardhi ya Ndung’u kuagiza kuwa ardhi hiyo irejeshwe chini ya umiliki wa Kitale school.