MBINU ZA UPANGAJI UZAZI ZAKUMBATIWA POKOT MAGHARIBI.
Idadi kubwa ya kina mama katika kaunti ya Pokot magharibi wamekumbatia mbinu za kisasa za upangaji uzazi.
Haya ni kulingana na utafiti ulioendeshwa na shirika la Performance Mornitoring Action PMA ambao umeonyesha kuwa kufikia sasa ni asilimia 26 ya wanawake ambao wanatumia mbinu hiyo ikilinganishwa na mwaka 2014 ambapo ilikuwa asilimia 13.
Mshauri mkuu katika shirika hilo Mary Thiong’o amesema kuwa asilimia 60 ya kina mama ambao hawatumii mbinu hizo wanasema kuwa hawahitaji mpango huo na kuwa hawako katika hatari yoyote kwa kukosa kutumia mbinu za kupanga uzazi.
Hata hivyo Thiong’o amesema kuwa tamaduni na mila za kijamii zimesalia changamoto katika kuwashawishi kina mama wengi katika kaunti hii kutumia mbinu za kisasa za upangaji uzazi.