MATOKEO YA KCSE YAENDELEA KUSHEREHEKEWA POKOT MAGHARIBI


Walimu wa shule mbali mbali katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameendelea kupongeza matokeo bora katika mtihani wa kitaifa kwa kidato cha nne KCSE ambayo yalitangazwa jumatatu na waziri wa elimu prof. George Magoha.
Akizungumza kwa niaba ya mwalimu mkuu, mkuu wa mtaala katika shule ya upili ya wasichanaya Tartar Andrew barasa amesema licha ya kuwa shule hiyo haikuafikia viwango ambavyo walikuwa wameweka, matokeo ya mwaka huu yaliimarika ikilinganishwa na yale ya mwaka 2019 ikizingatiwa watahiniwa 192 walipata alama za kuwawezesja kujiunga na vyuo vikuu.
Ni kauli ambayo pia imetolewa na mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Totum Rael alotum ambaye amesema matokeo ya shule hiyo yameimarika kutoka point 3.2 mwaka 2019 hadi pointi 4.7 mwaka huu huku wanafunzi wawili wakipata alama za kuwawezesha kujiunga na chuo kikuu kwa mara ya kwanza.
Hata hivyo mwalimu mkuu wa shule ya upili ya our lady of peace Pser Maiyo siritalewo ametetea matokeo ya shule yake akishikilia kuwa ndiyo matokeo halisi kinyume na matokeo ambayo ilipata katika miaka ya awali, baada ya shule hiyo kupata pointi 3.6 katika mtihani huo.