MATAYARISHO YOTE YA MCHUJO YA CHAMA CHA UDA YAMEKAMILIKA KAUNTI YA TRANSNZOIA


Chama cha UDA kikijitayarisha kwa kura ya mchujo kuanzia juma lijalo, chama hicho kimefanya mkutano na usimamizi wa uchaguzi na wagombezi viti 134 wa chama hicho kwenye nyadhifa mbalimbali mjini Kitale.
Wakiongozwa na mshirikishi wa chama cha UDA Kaunti ya Trans Nzoia Philemon Kirwa amesema matayarisho yote yamekamilika na wagombezi wote wameonyesha imani kwa matayarisho yaliowekwa na usimamizi wa chama hicho akiahidi kura ya haki na uwazi kwa wagombea wote.
Wakati huo huo kirwa amedokeza kuwa chama hicho kifanya kura ya mchujo wa chama hicho kwenye maeneo bunge manne na kwenye viti 23 ya wagombeaji wa kiti cha uwakilishi wadi na wakilishi wa akina Mama, akisema kwenye viti vilivyo salia chama hicho aidha kimekuwa na mgombea mmoja pekee au kumwekuwa na maelewano baina ya wawaniaji viti
hivyo.