MASOMO KATIKA SHULE ZILIZOATHIRIKA NA UTOVU WA USALAMA BARINGO KUREJELEWA JUMA HILI.

Shule zote zilizofungwa katika kaunti ya Baringo kufuatia ukosefu wa usalama zinatarajiwa kufunguliwa jumatano wiki hii.
Hii ni kufuatia agizo la serikali ambayo imeahidi kuhakikisha kwamba wanafunzi wanapata usalama wa kutosha na vyakula wakiwa shuleni.
Tangu kuanza muhula wa kwanza juma lililopita zaidi ya wanafunzi alfu 5 wamekosa kurejea shuleni.
Miongoni mwa shule ambazo zimeathirika zaidi ni Kapkechil, Karne, Koitiliel tuyiotich, Kapindesum, Kasiela, Arabal, Sinoni, Chebinyinyi, Embasos, Kosile, Chemoek, Kagiri, Ng’aratuko miongoni mwa shule zingine.