MASKWOTA WA CHEPCHOINA WATISHIA KUISHITAKI SERIKALI ICC.
Maskwota waliofurushwa kwenye ardhi yenye utata ya chepchoina mpakani pa kaunti hii ya Pokot Magharibi na kaunti jirani ya Trans nzoia wametishia kuishtaki serikali kwenye mahakama ya jinai mjini the hague wakidai kuhangaishwa licha kufurushwa mwaka jana kutoka kwenye ardhi yao.
Maskwota hao wanadai kuhangaishwa na maafisa wakuu wa serikali huku kesi zao zikitupiliwa mbali mahakamani wakitafuta haki.
Hiyo jana mahakama ya kitale imetupilia mbali ombi lao la kuitaka iamuru warejeshwe kwenye ardhi yao hadi pale kesi waliyowasilisha isikizwe.
Maskwota hao wanasema kuwa sasa hawana imani na idara ya mahakama huku wakimtaka rais uhuru kenyatta kusuluhisha swala hilo kabla ya kustaafu.