MASKWOTA CHEPCHOINA WATAKA MAKAO YA KUDUMU.
Maskwota wanaoishi kwenye ardhi yenye utata ya Chepchoina katika kaunti ya Trans nzoia wamemwomba rais Uhuru Kenyatta kuwapa makao ya kudumu kabla ya kukamilika muhula wake mwaka ujao.
Maskwota hao wengi wao wakiwa akina mama na wakongwe wamesema kuwa wanapitia mahangaiko tele na kuwa hawana uridhi wa kuwapokeza wanao.
Mwenyekiti wa muungano wa kiboroa squatters alliance Ainea Masinde amesema kuwa kwa mujibu wa katiba kila mkenya ana haki ya kuishi popote nchini akitoa wito kwa idara ya upelelezi DCI na tume ya NCIC kuwachunguza watu wanaotoa semi za chuki taifa linapokaribia uchaguzi mkuu.