MASHIRIKA YA KIJAMII POKOT MAGHARIBI YAENDELEZA UHAMASISHO DHIDI YA VIJANA KUTUMIKA KISIASA.


Mashirika mbali mbali ya kijamii katika kaunti hii ya Pokot magharibi yanaendelea uhamasho kwa vijana dhidi ya kutumika vibaya na wanasiasa hasa msimu huu wa siasa za uchaguzi mkuu wa mwezi agosti mwaka huu.
Kulingana na afisa katika shirika la Sominerec Elisha Ombwai mara kwa mara katika msimu wa siasa za uchaguzi vijana ndio hulengwa zaidi na wanasiasa kutekeleza visa vya uovu hasa dhidi ya wapinzani wao ili kujinufaisha kisiasa.
Akizungumza baada ya kukutana na baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka maeneo ya mipakani pa kaunti hii, Ombwai amesema kuwa wanalenga kuwaelimisha vijana kuhusu umuhimu wa kujihusisha na maswala yatakayowanufaisha na kuepuka kutumika kisiasa.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na naibu kamishina eneo la Chesogon Naphtali Korir ambaye aidha amesema kuwa wanalenga pia kuwatumia vijana kuwa mabalozi wa amani ili kueneza ujumbe wa amani hasa maeneo hayo ya mipakani.