MASHIRIKA NA SEFA NA NRT YAENDELEA KUWANUFAISHA WAKULIMA POKOT MAGHARIBI.


Wakulima eneo la orolwo, eneo bunge la Sigor katika kaunti hii ya Pokot magharibi wamenufaika na mbegu za mimea mbali mbali kutoka kwa shirika la sefa kwa ushirikiano na lile la ustahimilivu ambayo yamekuwa yakiendeleza miradi mbali mbali kaunti hii kwa manufaa ya wakulima.
Akizungumza baada ya shughuli ya kuwakabidhi takriban wakulima alfu moja mbegu hizo ikiwemo za ndengu, kunde, dania miongoni mwa zingine, afisa katika shirika la sefa Beatrice hadeny amesema lengo kuu ni kuimarisha uzalishaji pamoja na kuhakikisha lishe bora miongoni mwa wakazi wa kaunti hii ya pokot magharibi.
Hadeny ametoa wito kwa wakulima kutumia mvua inayoshuhudiwa kwa sasa katika kaunti hii kupanda mimea hiyo huku akiwashauri dhidi ya kuuza mazao yote kwani lengo kuu la mradi huo ni kuhakikisha wanatumia mazao hayo kama chakula katika kuhakikisha afya bora.
Kwa upande wake waziri wa kilimo na mifugo katika kaunti hii Geofrey Lipale amepongeza mashirika hayo kwa juhudi za kuhakikisha mkulima kaunti hii anawezeshwa huku akiahidi kuwa wizara yake itashirikiana nao kikamilifu kuhakikisha wakulima wengi wananufaika.