MASHARIKA YA KIJAMII YATAKA HAKI ZA WATOTO KULINDWA.
Ili kuhakikisha watoto na kinamama wanaodhulumiwa katika jamii wanapata haki, ni sharti kuwepo mikakati ya kudumu na ushirikiano baina ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayoangazia maswala ya watoto pamoja na idara mbalimbali za serikali.
Haya yamebainika baada ya kikundi cha mashirika ya kijamii na maafisa wa idara mbalimbali chini ya muungano wa Child Protection Network kaunti ya Pokot magharibi kuzuru wenzao katika kaunti ya Turkana kujifunza jinsi yanavyoshughulikiwa maswala ya watoto katika kaunti hiyo.
Mwenyekiti wa mashirika hayo Carolyne Menach amesema serikali ya kaunti ya Pokot magharibi inapasa kuiga mengi kutoka kaunti ya Turkana na kujenga makao ya kuwahifadhi watoto na kinamama wanaopitia dhuluma mbalimbali katika jamii.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na Mercy Cheruto kutoka shirika la World vision ambaye amesisitiza umuhimu wa kuwepo ushirikiano baina ya idara mbalimbali wanaposhugulikia kesi za watoto.