MARUFUKU YA ‘KWARAKWARA’ YAUNGWA MKONO NA VIONGOZI POKOT MAGHARIBI.


Hatua ya naibu kamishina eneo pokot kaskazini kaunti hii ya Pokot magharibi kupiga marufuku michezo inayojulikana kama nasa kwarakwara eneo hilo imeendelea kupongezwa na baadhi ya viongozi katika kaunti hii ya pokot magharibi.
Spika wa bunge la kaunti hii ya Pokot magharibi Catherine Mukenyang amesema kuwa hatua aliyochukua kamishina huyo ilifaa kwani watoto wengi wa kike wameathirika pakubwa kwa kuhudhuria hafla hizo ambapo wengi wao wameishia kupachikwa mimba.
Aidha Mukenyang amesema kuwa hafla hizo zimepelekea kudorora maadili miongoni mwa jamii kutokana na kupuuzwa tamaduni na mila za jamii ya pokot huku pia akitoa wito kwa wakazi kuandaa shughuli zao ikiwemo sherehe nyakati za mchana.