MAPUUZA YATAJWA KUCHANGIA VISA VINGI VYA DHULUMA ZA JINSIA POKOT MAGHARIBI.


Visa vingi vya dhuluma za jinsia vinavyoendelea miongoni mwa jamii katika kaunti hii ya Pokot magharibi vimekosa kuripotiwa kutokana na mapuuza baadhi ya waathiriwa kuhofia usalama wao iwapo wataripoti visa hivyo hali ambayo inapelekea wengi kukosa haki.
Haya ni kwa mujibu wa afisa katika shirika la DSW Kenya Peris Motoyo ambaye aidha amesema kuwa waathiriwa wengi wa visa hivi hasa maeneo ya mashinani wanakosa kupata haki kutokana na visa vingi kama hivyo kusuluhishwa nyumbani.
Hata hivyo amesema juhudi za mashirika ya kijamii kukabiliana na dhuluma za kijinsia zinalemazwa na changamoto ya uhaba wa raslimali za kufanikisha hilo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtandao wa kushughulikia maswala ya watoto katika kaunti hii ya Pokot magharibi child protection network Carolyne Menach amesema wameanzisha kampeni za kuwahamasisha vijana vijijini pamoja na shule mbali mbali ili kukabili visa hivi.