GAVANA WA POKOT MAGHARIBI ATARAJIWA KUZINDUA MAONYESHO YA KILIMO HIVI LEO


Licha ya kuwapo kwa vitisho vya janga la korona nchini, wizara ya kilimo na mifugo katika kaunti ya Pokot Magharibi leo asubuhi ya leo inatarajiwa kuzindua rasmi maonyesho ya kilimo yatakayofanyika kwa siku tatu katika uwanja wa maonyesho ya Kishaunet.
Akizungumza na wanahabari kabla ya uzinduzi huo , waziri wa kilimo na mifugo katika kaunti hiyo Geoffrey Lipale amewataka wakazi wa kaunti hiyo pamoja na wageni wengine kuwa huru kuhudhuria maonyesho hayo huku akitoa hakikisho kwamba wizara ya afya imeweka mikakati kabambe ya kuzuia maambukizi ya virusi vya korona miongoni mwa hadhira itakayohudhuria. Amewaomba watu wote watakaohudhuria kufuata masharti yote ya kuzuia korona likiwamo kuvaa barakoa.

Bw. Lipale amesema lengo kuu la maonyesho hayo ni kuimarisha uzalishaji wa mifugo na mimea katika kaunti ya Pokot Magharibi.