MALUMBANO YA UONGOZI FORD KENYA YAATHIRI MAENDELEO TRANS NZOIA NA BUNGOMA.
Kaunti za Trans nzoia na Bungoma hazijakuwa zikifanya vyema kutokana na malumbano ya uongozi katika chama cha Ford Kenya ambapo magavana wote wawili Patrick khaemba na wyclife wangamati wamechaguliwa kwa chama hicho.
Akihutubu wakati wa hafla ya mchango wa ununuzi wa kipande cha ardhi kinachonuiwa kupanua ujenzi wa zahanati ya Nabeki Cherubai kwenye eneo bunge la Endebes waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa amesema wakati umefika kwa viongozi walio mamlakani katika kaunti hiyo kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.
Aidha wamalwa amesema sekta ya afya ndiyo iliathirika mno na kuwa ni kinaya kwa magari ya polisi kutumika kuwasafirisha wagonjwa na kina mama wajawazito kwa kukosa ambulansi.