MALUMBANO BAINA YA RAIS NA NAIBU WAKE YAKASHIFIWA VIKALI.
Wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi wameshutumu majibizano ambayo yanaendelea kushuhudiwa baina ya rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wakiyataja kuwa hatari hasa wakati huu ambapo taifa linaelekea katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti.
Wakiongozwa na Henry Sonko wakazi hao wamesema kuwa huenda majibizano hayo yakapelekea migawanyiko miongoni mwa wananchi wakimtaka rais Kenyatta kujitenga na majibizano hayo kwani yeye hayuko katika kinyang’iro cha urais katika uchaguzi wa mwezi agosti.
Aidha wakazi hao wamemtetea naibu rais kutokana na madai kwamba nusra amzabe kofi rais Kenyatta aliyetaka kujiondoa kinyang’anyironi baada ya mahakama kufutilia mbali uchaguzi mkuu wa mwaka 2017 wakisema Ruto alikuwa akitetea alichofanyia juhudi kupata.
Wakati uo huo wakazi hao wamekashifu manifesto ya mgombea urais wa chama cha the Roots George wajakoya hasa kuhalalisha upanzi wa bangi nchini wakisema kuwa ni ya kuwapotosha vijana pamoja na kuongeza visa vya utovu wa usalama nchini.