MALI YENYE DHAMANI ISIYOJULIKANA YAHARIBIWA BAADA YA BWENI KUTEKETEA


Mali yenye dhamani isiyojulikana imeteketea usiku wa kuamkia leo katika shule ya upili ya Kitur kaunti ya Baringo baada ya moto mkubwa kuteketeza bweni moja la shule hiyo.
Maafisa wa usalama shuleni humo waliwaita maafisa wa polisi ambao kwa ushirikiano na wazima moto kutoka kaunty ya Baringo walifanikiwa kuuzima moto huo.
Wanafunzi wote hata hivyo wako salama kufuatia kisa hicho cha saa tano za usiku chanzo cha moto hakijabainika japo uchunguzi wa kina umeanzishwa.