MAKUNDI YA WAKULIMA POKOT MAGHARIBI YANUFAIKA NA UFADHILI


Makundi 114 ya ukulima katika kaunti hii ya Pokot magharibi yamepokea ufadhili wa shilingi milioni 96 kupitia mradi wa climate smart ili kuwafaidi kwenye ukulima wao..
Akizungumza na wanahabari katika hafla iliyoandaliwa katika uwanja wa makutano, waziri wa kilimo katika kaunti hii ya Pokot magharibi Lipale Geofrey amesema kuwa makundi hayo yalikuwa yamepokea fedha hizo kwa awamu ya kwanza hii ikiwa ni ya awamu ya pili na ya tatu itakayo wawezesha kufanya ukulima wao.
Lipale aidha amesema kuwa ufadhili huo umetoka kwa benki ya dunia akisema kuwa imepitia katika bajeti ya serikali ya kaunti hii.
Ni hafla ambayo iliongozwa na gavana wa kaunti ya Pokot magharibi Prof. John Lonyangapuo ambaye alisisitiza kujitolea serikali yake katika kuyawezesha makundi ya wakulima.