MAKUNDI YA KINA MAMA TRANS NZOIA YALALAMIKIA UGUMU WA KUPATA MIKOPO.


Makundi ya akina mama eneo la cherang’ani katika kaunti ya Trans nzoia yamelalamikia ugumu wa kupata mikopo hali wanayodai kuwa imesababishwa na kuwepo masharti mengi kabla ya kupata mikopo hiyo.
Wakiongozwa na Zainab Keter, kina mama hao wamesema kuwa wengi wao wanaishi katika hali ya ufukara hali inayowapelekea wengine wao kujitoa uhai kutokana na msongo wa mawazo na kuwa njia ya pekee ya kuwasaidia ni kupitia mikopo hiyo.
Ni kauli ambayo imetiliwa mkazo na viongozi wa akina mama katika kaunti hiyo wakiongozwa na Grace Were ambao wametayataka mashirika husika kulegeza baadhi ya masharti hayo.