MAKASISI KAUNTI YA TRANSNZOIA WAOMBWA KUTOJIHUSISHA NA MASWALA YA SIASA NA BADALA YAKE KUWA MFANO MWEMA


Wito umetolewa kwa kanisa kuonyesha mfano mwema kwa kujiepusha na siasa za ukabila siasa za tofauti wa vyama vya kisiasa.
Akihutubu kwenye Kanisa la ACK St Luke’s mjini Kitale Ole Ndiema amesema wakati mwingi kanisa hulalamikia wanasiasa ufisadi na pesha za umma kupotea akiwataka kufanya uamuzi bora wa kuchagua viongozi walio na madili mema na wacha Mungu.
Wakati huo huo Ole Ndiema ambaye anawania kiti cha useneta Kaunti ya Trans Nzoia amesikitikia kukwama kwa miradi mingi ya maendelea walioanzisha kwenye awamu yake ya kwanza ikiwa ni pamoja na miradi ya afya kilimo na utoaji wa hatimiliki kwa wenyeji Kaunti ya Trans Nzoia.