MAKALI YA NJAA YAZIDISHA HOFU TIATI, BARINGO.


Shirika la msalaba mwekundi nchini (kenya red cross) limeelezea wasi wasi wa kuongezeka kwa idadi ya wakenya wanaokabiliwa na tatizo la ukosefu wa chakula iwapo mvua haitashuhudiwa maeneo tofauti nchini.
Akiongea katika eneo la riongo, eneo bunge la Tiaty kaunti ya Baringo wakati wa mpango wa kununua mifugo kutoka kwa wakazi, afisa wa shirika hilo michael ayabei amesema kuwa kwa sasa wakenya M 4.1 wanakabiliwa na uhaba wa chakula.
Ayabei amesema kuwa kaunti 14 kati ya 47 nchini ndizo zilizoathirika zaidi na kiangazi cha muda mrefu na mpango wa kununua mifugo kutoka kwa wakazi ni moja ya mikakati ya serikali kukabili athari za ukame.
Kwa upande wake naibu kaunti kamisha eneo la Tiaty magharibi Josiah Odongo amesema kuwa wanaolengwa kwenye mpango wa ugavi wa chakula ni watu kutoka familia masikini zaidi na pia baadhi ya shule ili kuzuia visa vya wanafunzi kukosa kuhudhuria masomo yao.