MAKALI YA NJAA YAZIDI KUSHUHUDIWA POKOT MAGHARIBI.

Takriban nyumba alfu 37 ambazo zimeathiriwa na baa la njaa zimefikiwa na idara ya majanga katika kaunti hii ya Pokot magharibi.
Akithibitisha haya msimamizi wa idara hiyo katika kaunti hii ya Pokot magharibi Dkt Michael ayabei amesema kuwa zaidi ya familia alfu 37 zimepokezwa msaada wa chakula huku zaidi ya familia alfu 16 zikikabidhiwa fedha taslimu za kuwasaidia kujikimu katika kipindi hiki kigumu.
Ayabei amesema kuwa mikakati mbali mbali ambayo inawekwa na idara hiyo kuwasaidia wakazi wa maeneo mbali mbali ya kaunti hii kukabili njaa imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya ukame ambao unashuhudiwa kila mara.
Ametoa wito kwa wahisani zaidi kujitokeza kusaidia katika juhudi za kuwasaidia wakazi wa kaunti hii ambayo inashuhudia idadi kubwa ya wanaokabiliwa na makali ya njaa.