MAJIBIZANO YAENDELEA KUSHUHUDIWA KATI YA GAVANA NA SENETA WA POKOT MAGHARIBI.


Seneta wa kaunti hii ya pokot magharibi Samwel Poghisio ameshutumu gavana wa kaunti hii John Lonyangapuo kutokana na kauli yake kuwa ndiye aliyemsaidia kuinuka kisiasa hata kufikia viwango vya sasa.
Akizungumza na kituo hiki Poghisio amesema kuwa amekuwa katika ulingo wa siasa kwa kipindi kirefu akimsuta gavana Lonyangapuo kwa kauli yake aliyoitaja kuwa matusi kwa viongozi wenza wa kisiasa na jamii ya kauti hii kwa ujumla.
Poghisio sasa anatoa wito kwa wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi kuwa makini na viongozi ambao watawachagua katika uchaguzi mkuu ujao na kuwachagua viongozi wenye maadili, huku akimlaumu lonyangapuo kwa kutowajibika licha ya kutengewa bajeti kubwa.
Akizungumza katika hafla moja siku chache zilizopita, gavana lonyangapuo alismuta Poghisio kwa kile alidai kushinikiza kufanyiwa uchunguzi na tume ya kukabili uafisadi eacc licha ya kuwa ndiye aliyemsaidia kurejea katika ulingo wa kisiasa.