Maimamu wapinga hatua ya mkuu wa DCI George Kinoti
Baraza la maimamu katika kaunti ya Uasin Gishu limeeleza kusikitishwa na hatua anayotaka kuchukua kiongozi wa idara ya upelelezi DCI George Kinoti kuchunguza kesi za ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2007/2008,likisema huenda hilo likatatiza amani katika maeneo tofauti nchini.
Baraza hilo likiongozwa na mwenyekiti Shekhe Abubakar Bini linasema jamii hasa katika kaunti ya Uasin Gishu zilisameheana na hivyo zinaendelea kuishi kwa utangamano.Aidha wamesema kwamba Kinoti hafai kufufua mambo yaliyopita na yaliyozikwa kwenye kaburi la sahau.
Wakizungumza kule Eldoret wametaka wakaazi wa Uasin Gishu kuendelea kuishi kwa amani.