MAHAKAMA YAWEKA ZUIO LA MUDA KUTIMULIWA MUKENYANG.


Spika wa bunge la kaunti hii ya Pokot magharibi Catherine Mukenyang amepata afueni ya muda baada ya mahakama kuu ya Eldoret kusitisha kwa muda uamuzi wa bunge hilo kumwondoa mamlakani.
Jaji wa mahakama hiyo Olga sewe alitoa agizo la muda kusitisha kuondolewa spika huyo kutokana na ombi la dharura alilowasilisha kupinga uamuzi wa kuondolewa kwake.
Mukenyang alimshitaki mwakilishi wadi ya Edough Evanson Lomaduny aliyewasilisha hoja ya kumwondoa pamoja na bunge la kaunti hii kwa kujadili hoja iliyomwondoa kwa kile amedai ni kwa njia haramu.
Akitoa agizo la kusitisha kuondolewa kwake Mukenyang, jaji Sewe aliwaagiza washitakiwa kujibu malalamishi hayo ndani ya muda wa siku saba.
Mukenyang alibanduliwa mapema mwezi huu kwa matumizi mabaya ya afisi na ukiukwaji wa sheria miongoni mwa tuhuma nyingine baada ya waakilishi wadi 25 kupiga kura kuunga mkono kuondolewa kwake huku 7 wakipinga hoja hiyo.