MAHAKAMA YAWAPA AFUENI MASKWOTA KAPSITWET TRANS NZOIA


Maskwota wa Kapsitwet Kaunti ya Trans Nzoia wamesifia uamuzi wa mahakama ya Kitale kwa kurejesha shamba la ekari alfu nne (4000) baada ya kumshitaki aliyekuwa Rais wa Pili Daniel Moi,marehem Nicholus Biwot,Joshua Kulei na marehenu Abraham Tanui.
Wanne hao walishitakiwa na Maskwota 250 waliofurushwa kwa Shamba la Kapsitwet baada Mzungu George Baba kuachia iliyokuwa Serikali ya Daniel Moi ili kuwapa makao lakini mabwenyeye wakanyakua shamba hilo.
Wakiongozwa na charles opondo wanaharakati hao wamemshukuru Mungu na Mahakama kwa kufanya haki baada ya kesi hiyo kudumu kotini kuanzia mwaka wa 2006.
Hata hivyo Boniface Telewa na Nick Musungu wakitoa onyo kwa Maskwota hao, huku wakishukuru Wakili wao Fredrick Musungu.
Wakati huo huo mahakama hiyo imeondolea gharama wale walionunua Shamba hilo pasipo ufahamu.