MAHAKAMA KUU INATARAJIWA KUJENGA MAHAKAMA ZAIDI ENEO LA ALALE NA SIGOR KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI
Idara ya mahakama itajitolea kuhakikisha kuwa wakenya wote wanapata haki kwa usawa hasa katika jamii ambazo zilitengwa kwa muda mrefu nchini.
Akizungumza baada ya kuzindua rasmi jengo la mahakama ya Kapenguria katika kaunti hii ya pokot magharibi, jaji mkuu Martha Koome amesema kuwa idara ya mahakama imeweka mikakati ambayo inalenga zaidi uwezo wa kufikia haki jamii za wachache na wale waliotengwa kwa muda mrefu.
Kwa upande wake gavana wa kaunti hii John Lonyangapuo ametoa wito kwa Koome kuidhinisha kurejeshwa kesi ambazo ziliwasilishwa kwa mahakama za Kitale na Eldoret na wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi ili zishughulikiwe katika mahakama kuu ya Kapenguria.