MAGOHA ATAKIWA KUFUATILIA MAAGIZO ANAYOTOA KATIKA SEKTA YA ELIMU.
Viongozi wa kisiasa katika kaunti ya Trans nzoia wamemtaka waziri wa elimu Prof. George magoha kufuatilia maagizo anayotoa ili kuwaepushia wazazi mahangaiko ambayo wanapitia kulipa karo.
Mwanasiasa Anthony Makan kutoka eneo la Saboti kaunti hiyo ya Trans nzoia amesema kuwa asilimia kubwa ya walimu wakuu wamekataa kushauriana na wazazi ambao hawajakamilisha karo na badala yake wamewatuma wanafunzi hasa watahiniwa nyumbani.
Wakati uo huo Makan ambaye pia ametangaza nia ya kugombea kiti cha mwakilishi wadi eneo la Saboti amewarai vijana kutokubali kutumika na wanasiasa kuzua vurugu.