MAGOHA ASHUTUMIWA KWA KUSEMA WAZAZI WATAGHARAMIA UHARABIFU SHULENI.

Na Benson Aswani
Wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi wametofautiana vikali na kauli ya waziri wa elimu Prof. George Magoha kuwa serikali haitogharamia ujenzi wa majengo ya shule ambayo yanateketezwa na wanafunzi na badala yake jukumu hilo kuachiwa wazazi.
Wakizungumza na kituo hiki wakazi hao wamesema kuwa kauli hiyo ya waziri magoha ni kejeli kwa wazazi kwani hamna mzazi ambaye amemshauri mwanaye kuteketeza majengo ya shule, wakimtaka Magoha kutafakari tena kauli yake.
Wakazi hao wamedai huenda waziri Magoha ana njama fiche dhidi ya wazazi wakisema kuwa badala ya wazazi kusukumiwa mzigo huo uchunguzi unapasa kufanywa na mwanafunzi yeyote atakayepatikana na hatia ya kuteketeza jengo la shule anafaa kuchukuliwa hatua za kisheria.