MAGOHA ASHUTUMIWA KWA AGIZO LA KUWATUMA WANAFUNZI NYUMBANI KUTAFUTA KARO.


Hisia mseto zimeendelea kuibuliwa miongoni mwa viongozi na wanachi kwa jumla nchini kufuatia agizo la waziri wa elimu prof. George magoha kuwataka walimu wakuu kuwatuma nyumbani wanafunzi ambao hawajakamilisha kulipa karo.
Mbunge wa Kapenguria kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Moroto ameilaumu wizara ya elimu kwa tangazo lake la awali ambapo waziri Magoha aliwaonya walimu dhidi ya kuwatuma nyumbani wanafunzi hali ambayo iliwafanya wazazi wengi kutokuwa na bidii ya kutafuta karo.
Aidha Moroto amewataka wakuu wa shule kuwa na subira na kutowatuma wanafunzi nyumbani, huku akilaumu kukithiri ufisadi miongoni mwa maafisa wa serikali hali ambayo amesema imechangia hali ngumu ambayo wakenya wanapitia kwa sasa kando na athari za janga la corona.
Hata hivyo mwakilishi kina mama katika kaunti hii ya pokot magharibi Lilian Tomitom amewataka wazazi kujikaza na kulipa kiwango fulani cha karo wakati wanapoendelea kusubiri fedha ambazo zinatolewa na serikali huku akitaka wadau kuharakisha kutoa fedha hizo.