MAGOHA ASHUTUMIWA KWA AGIZO LA KUWATUMA NYUMBANI WANAFUNZI.


Hisia mseto zimeendelea kuibuliwa kufuatia hatua ya waziri wa elimu profesa George Magoha kuwaagiza walimu wakuu kuhakikisha kuwa wazazi wanalipa karo kwa kuwatuma nyumbani wanafunzi ambao hawajakamilisha karo.
Wakiongozwa na Henry ngata wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi wameshutumu hatua hiyo wakisema Magoha hakustahili kutoa kauli hiyo hasa ikizingatiwa hali ngumu ambayo wazazi wanapitia wakati huu kufuatia athari zilizosababishwa na janga la corona.
Wamesema kuwa wazazi wanapaswa kupewa muda wa kutafuta karo kwani wanafahamu kuwa ni jukumu lao kulipa karo ya wanao na hamna mzazi ambaye amekataa kutekeleza jukumu hilo.