MAGAVANA WAPYA WANZA RASMI KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO.


Siku chache tu baada ya magavana 45 kula kiapo na kuahidi kufanyia wananchi kazi sasa magavana hao wameanza rasmi majukumu yao.
Ikiwa ni siku ya kwanza kuingia ofisini tangu kuchaguliwa kwake gavana wa kaunti hii ya pokot magharibi simon kachapin amezuru ofisi mbali mbali katika kaunti hii na kukagua wafanyikazi wa kaunti jinsi wanavyofanya kazi ikizingatiwa yeye ndiye aliyekuwa gavana wa kwanza kabla ya kumpisha gavana ambaye ameondoka lonyangapuo.
“Niko katika hali ya kujifahamisha na shughuli za kaunti na kukagua jinsi wafanyikazi wanafanya kazi katika afisi za serikali na pia kuyakagua majengo niliyojenga. Kwa hivyo nafurahia kuwa kazini kwa siku ya kwanza.” Alisema.

Aidha kachapin ametumia fursa hiyo kuitoa onyo kali kwa wafanyikazi wa kaunti wanaozembea kazini hasa wale ambao hawajarejelea majukumu yao kufikia sasa kwamba watachukuliwa hatua kali za kisheria.
“Ninatoa wito kwa wale ambao hawajaripoti kazini watoke nyumbani waje wawahudumie wananchi. Na yule ambaye hatapatikana afisini basi atachukuliwa hatua za kisheria na hata kama serikali imebadilika nataka wafanyikazi wote waendelee kutoa huduma.” Alisema Kachapin.
Wakati uo huo gavana Kachapin amekikariri kwamba chini ya uongozi wake taratibu za kisheria zitafuatwa kabla ya kumwajiri afisa yeyote katika ofisi za kaunti.