MAFUNZO KUHUSU LISHE BORA YAZINDULIWA POKOT MAGHARIBI.
Shirika la kushughulikia maswala ya watoto UNICEF limezindua rasmi mpango wa kutoa mafunzo kwa kina mama kuhusu lishe bora kwa jina NICHE ili kuzuia visa vya kudumaa miongoni mwa watoto katika kaunti hii ya Pokot magharibi.
Akizungumza baada ya kuzindua mpango huo katika zahanati ya Psigirio eneo bunge la Kapenguria, afisa katika shirika hilo Elizabeth cherop amesema kuwa mpango huo unalenga watoto alfu 1,400 kaunti hii ambapo maafisa husika watakuwa wakizuru kila nyumba mara mbili kwa mwezi kutoa mafunzo hayo.
Mshirikishi wa maswala ya afya na lishe bora katika shirika la Action against hunger Jemimah Hamadi amesema kauti ya pokot magharibi ni moja ya kaunti za maeneo kame ambazo zina viwango vya juu vya utapia mlo licha ya kupungua kutoka asilimia 45 katika miaka ya awali hadi asilimia 35.1 ya sasa mpango huo utasaidia kukabili.
Kwa upande wake msimamizi wa idara ya watoto kaunti hii Philip Okopa amesema kuwa mpango huo unawalenga zaidi wakazi ambao wako kwenye mpango wa inua jamii ambao hupata shilingi alfu 4 kila baada ya miezi miwili ambapo sasa watakuwa wakipokea shilingi alfu tano ambapo wataongezewa alfu moja zitakazofanikisha mpango wa lishe bora kwa watoto wa chini ya miaka miwili.