MADAKTRAI KAUNTI YA BUSIA WASHAURIWA KUTOSHIRIKI MGOMO AMBAO UNATARAJIWA KUANZA JUMATATU WIKI IJAYO
Gavana wa kaunti ya Busia Sospeter Ojamong amewarai madaktari kwenye kaunti yake kutoshiriki mgomo wa kitaifa mabao unatarajiwa kung’oa nanga siku ya jumatatu wiki ijayo huku akiwashauri washiriki mazungumzo kuhusiana na matakwa yao.
Akizungumza kwenye kaunti yake, gavana Ojamong amesema kuwa kaunti hiyo imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba inatekeleza baadhi ya malalamishi ya madaktari kama njia moja ya kuboresha mazingira ya kufanyia kazi.
Ojamong’ hata hivyo amekiri kutokuwa na fedha za kuwalipa madaktari hao.
Chama cha kitaifa cha madaktari KMPDU kilikuwa kimetoa makataa mbayo yatakamilika siku ya jumapili usiku wakilalamikia Bima ya afya, mazingira duni ya kufanyia kazi, marupurupu na ukosefu wa vifaa vya kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.