MADAI YA UFISADI YAIBULIWA KATIKA USAJILI WA MAKURUTU WA KDF POKOT MAGHARIBI.


Baadhi ya viongozi wa kisiasa katika kaunti hii ya Pokot magharibi wamelalamikia zoezi la usajili wa makurutu wa KDF ambalo limekuwa likiendelezwa katika kaunti hii.
Akizungumza baada ya uzinduzi wa kituo cha polisi cha kacheliba kilichokarabatiwa kwa ufadhili wa fedha za CDF, mbunge wa eneo hilo Mark Lumnokol amedai kuwa zoezi hilo liligubikwa na ufisadi na kuwa wote waliofuzu walichukuliwa baada ya kutoa hongo.
Lumnokol amewataka wakazi wa eneo hilo kuwa waangalifu linapotangazwa zoezi hilo ili kuhakikisha kuwa visa vya ufisadi haviripotiwi kwani wengi wanaopewa fursa hizo ni watu kutoka jamii zilizo na uwezo mkubwa kifedha huku wanaofuzu wakiachwa nje.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na mbunge wa Sigor Peter Lochakapong ambaye aidha ametaka kuchunguzwa idara ya usajili wa watu kwa kile amedai inahusika ufisadi kwani wengi wanaosajiliwa katika zoezi hilo si wakazi wa maeneo husika.