MADAI YA LONYANGAPUO YA KUIMARIKA SEKTA YA ELIMU CHINI YA UTAWALA WAKE YAPUUZILIWA MBALI NA VIONGOZI POKOT MAGHARIBI.
Baadhi ya viongozi wa kisiasa katika kaunti hii ya Pokot magharibi wamepuuzilia mbali kauli ya gavana John Lonyangapuyo kwamba sekta ya elimu katika kaunti hii imeimarika zaidi chini ya uongozi wake kutokana na hatua yake kuwekeza zaidi katika sekta hiyo.
Aliyekuwa gavan wa kaunti hii Simon Kachapin ambaye kwa wakati mmoja alihudumu kama naibu waziri wa elimu nchini, amesema kuwa viwango vya elimu kaunti hii vimeshuka mno hali anayoihusisha na utovu wa ushirikiano miongoni mwa wadau.
Aidha Kachapin ambaye anawania tena wadhifa wa ugavana kaunti hii kupitia chama cha UDA amemsuta gavana Lonyangapuo kwa kile amedai kutumia muda wake mwingi kuendeleza siasa za propaganda na kuyatelekeza maswala muhimu katika kaunti hii.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na seneta wa kaunti hii Samwel Poghisio ambaye aidha amesema serikali ya gavana lonyangapuo imefeli pakubwa katika usimamizi wa idara muhimu hali ambayo imeifanya kusalia nyuma ikilinganishwa na maeneo mengine nchini.