MACHIFU TRANS NZOIA WATAKIWA KUKABILI POMBE HARAMU.
Machifu katika maeneo mbali mbali ya kaunti ya Trans nzoia wametakiwa kushirikiana na wadau wengine katika idara ya usalama kaunti hiyo kuhakikisha kuwa ugemaji wa pombe haramu pamoja na utumizi wa dawa za kulevya miongoni mwa vijana unakabiliwa vilivyo.
Kamishina wa kaunti hiyo sam Ojwang amesema kuwa utovu wa usalama katika kaunti hiyo umechangiwa pakubwa na kukithiri utumizi wa dawa za kulevya miongoni mwa wakazi hali anayosema inastahili kukabiliwa.
Aidha ojwang amewaonya maafisa hao kuwa huenda hatua za nidhamu zikachukuliwa dhidi yao iwapo hawatatekeleza majukumu yao inavyopasa na badala yake kuruhusu kuendelea ugemaji pombe haramu maeneo yao ya uwakilishi huku akionya vikali maafisa watakaopatikana wakibugia pombe kuwa watafutwa kazi.