MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU JUMANNE YAKAMILIKA.


Masaa machache tu kabla ya uchaguzi mkuu wa jumanne juma hili tume ya uchaguzi IEBC imesema kuwa maandalizi yamekamilika kwa ajili ya uchaguzi huo.
Afisa wa tume hiyo eneo bunge la Kapenguria kaunti hii ya Pokot magharibi Enoch otara amesema kuwa tayari wamepokea vifaa vyote vitakavyotumika katika uchaguzi huo ikiwemo karatasi za kupigia kura pamoja na mitambo ya kiems.
Aidha amesema wadau husika katika uchaguzi huo tayari wamepokea mafunzo kuhusu jinsi uchaguzi huo unapasa kuendeshwa.
“Tumefanya maandalizi yetu vyema, tumetoa mafunzo kwa wadau wote ambao tutafanya nao kazi, tumepokea vifaa vyote vya kupigia kura ikiwa ni pamoja na karatasi za kupigia kura na mitambo ya KIEMS na sasa tuko tayari kwa shughuli hiyo.” Amesema Otara.
Wakati uo huo Otara amewahakikishia wakazi wa eneo bunge la Kapenguria kwamba changamoto mbali mbali ambazo zingeshuhudiwa katika uchaguzi huo ikiwemo tatizo la mtandao pamoja na usafiri zimeshughulikiwa.