MAAFISA WA POLISI WA KITUO CHA MARICH KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WANAWASAKA WANAUMME KUMI WALIOHUSIKA KWA KUMLAZIMISHIA MSICHANA MMOJA NDOA YA MAPEMA.

Maafisa wa polisi katika eneo la sigor kaunti hii ya pokot magharibi wanawatafta wanaumme kumi wanaosemekana kumdhulumu msichana mwenye umri wa miaka kumi na miwili aliyekataa kuolewa na mtu mzee mwenye umri mkubwa.
Inaarifiwa kwamba baba ya msichana huyo aliashirikiana na wanaumme wengine kumchapa ili akubali kuolewa kwa kuwa mzee huyo alikuwa ameshalipwa mahari ya ngombe kumi
Kulingana na ripoti katika kituo cha marich msichana huyo alitoroka wakati sherehe zilipokuwa zinafanyika kumkaribisha kuwa mke
Polisi wanasema mwathiriwa waliwaeleza kuwa alifanikiwa kutoroka baada ya wanaumme akiwamo aliyetaka kumuoa walikuwa wamelewa chakari
Mkuu wa polisi wa eneo hilo la sigor kaunti hii ya pokot magharibi benford surwa amesema kwamba washukiwa wanaotaftwa walikuwa pia wamepanga kumkeketa msichana huyo