MAAFISA WA EACC WACHUNGUZA MIRADI YA BUNGE LA POKOT MAGHARIBI


Maafisa wa tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC kutoka jijini Nairobi wamefika katika majengo ya bunge la kaunti hii ya pokot magharibi kukagua miradi ambayo imetekelezwa na bunge hilo.
Maafisa hao wanatarajiwa kukagua makazi ya spika wa bunge hilo pamoja na mghahawa ambao umejengwa na bunge hilo kutokana na madai kuwa taratibu zinazostahili kabla ya kutekeleza miradi hiyo hazikufwatwa kulingana na sheria.
Aidha maafisa hao wanatarajiwa kukagua jengo jipya la bunge la kaunti ambalo linajengwa kando na bunge la sasa.
Kumekuwepo na madai ya utumizi mbaya wa fedha katika miradi ambayo inatekelezwa na bunge hilo halia ambayo imevutia uchunguzi kutoka kwa tume hiyo.