LUMUNOKOL ASHUTUMU VURUGU ZILIZOSHUHUDIWA NASOKOL
Mbunge wa Kacheliba ambaye ni mwenyekiti wa chama cha UDA katika kaunti hii ya Pokot magharibi Mark Lumnokol ameshutumu kisa cha kupatikana mwanamke mmoja akitia saini makaratasi ya kupigia kura ya wawaniaji wa ugavana katika kaunti hii katika kituo cha Nasokol.
Kulingana na lumnokol huenda hatua ya kupatikana mwanamke huyo na karatasi hizo ilikuwa moja ya njama za mrengo pinzani kutekeleza kile alichodai kuwa wizi wa kura kutokana na hofu ya kushindwa katika uchaguzi ulioandaliwa jumanne.
Ametoa wito kwa wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi kuwa makini na kuripoti kisa chochote kisicho cha kawaida kwa maafisa wa polisi ili hatua mwafaka zichukuliwe.
Wakati uo huo lumnokol ametoa wito kwa viongozi wote ambao watashindwa katika uchaguzi huo kukubali matokeo jinsi yatakavyotangazwa ili kutoa nafasi kwa viongozi waliochaguliwa kuwahudimia wananchi.