LONYANGAPUO AWAHAKIKISHIA WAKAZI WA POKOT MAGHARIBI MAENDELEO


Gavana wa kaunti hii ya Pokot magharibi John Lonyangapuo amewahakikishia wakazi wa kaunti hii kuwa serikali yake imejitolea kuhakikisha inatimiza miradi ya maendeleokwa manufaa ya wakazi.
Akizungumza eneo la karenger kaunti ya Pokot Magharibi, baada ya kuzindua ujenzi wa zahanati pamoja na bwawa, lonyangapuo amesema kuwa serikali yake imeweka fedha za kutosha za kufanikisha miradi hiyo kulingana na manifesto yake.
Aidha Lonyangapuo amesema kuwa baadhi ya miradi ambayo ametekeleza eneo hilo ikiwemo ujenzi wa barabara, shule, kuleta umeme miongoni mwa mingine imepelekea upatikanaji wa amani hilo ambalo awali lilisheheni visa vya uvamizi.
Wakati uo huo Lonyangapuo amewahimiza wakazi wa kaunti hii kuendelea kushirikiana na serikali yake kwa kudumisha amani na pia kuzingatia swala la dini ili kufanikisha utekelezwaji wa miradi ya maendeleo.