LONYANGAPUO ATAKIWA KUTIMIZA AHADI YAKE KWA WAATHIRIWA WA MOTO KONGELAI.

Na Benson Aswani
Gavana wa kaunti hii ya Pokot magharibi John Lonyangapuo ametakiwa kutimiza ahadi yake ya kuwasaidia wafanyibiashara katika soko la Kongelai eneo bunge la Kacheliba waliokadiria hasara kufuatia mkasa wa moto ulioshuhudiwa katika soko hilo mwaka jana.
Wafanyibiashara hao wamesema kuwa mwaka mmoja tangu mkasa huo wa moto hawajapata msaada wowote licha ya kuahidiwa na gavana lonyangapuo kima cha shilingi milioni mbili za kuwasaidia kufufua biashara zao.
Wafanyibiashara hao wamesema kuwa walikuwa wakitegemea biashara hizo kwa riziki zao za kila siku ila sasa wengi wao wameshindwa kabisa kuinuka tena kutokana na hasara kubwa waliyokadiria kutokana na mkasa huo wa moto.