LONYANGAPUO ATAKA SEKTA YA ELIMU KUGHATULIWA KIKAMILIFU.


Gavana wa kaunti hii ya Pokot magharibi John Lonyangapuo amelalamikia pakubwa sehemu kubwa ya sekta ya elimu kusimamiwa na serikali kuu huku serikali za kaunti zikiachiwa kusimia elimu ya chekechea.
Akizungumza alipokutana na wakuu wa shule za upili kaunti hii katika makao makuu ya gavana, Lonyangapuo ametaka serikali za kaunti kuachiwa usimamizi wa sekta nzima ya elimu kwani zina uwezo na raslimali za kutosha kusimamia sekta hiyo.
Lonyangapuo amesema kuwa serikali za kaunti zimetengwa pakubwa katika sekta ya elimu licha ya kuwa zinawekeza pakubwa katika sekta hiyo hata kuliko serikali kuu.
Amesema licha ya juhudi za serikali hizo kuhakikisha sekta ya elimu inaimarishwa hazijakuwa zikinufaika na matunda ya juhudi hizo akitishia kusitisha ufadhili ambao serikali yake inatoa kwa sekta hiyo.