LONYANGAPUO ATAKA KUTUPILIWA MBALI SERA YA UHAMISHO WA WALIMU POKOT MAGHARIBI.
Na Benson Aswani
Gavana wa kaunti hii ya Pokot magharibi John Lonyangapuo ametaka sera ya uhamisho wa walimu kutoka kaunti hii ya pokot magharibi hadi maeneo mengine ya nchi kutupiliwa mbali.
Akizungumza wakati wa kuwasilisha matakwa ya jamii ya kaunti hii kwa kinara wa ODM Raila Odinga, Lonyangapuo amesema kuwa hatua hii imeathiri pakubwa viwango vya elimu hali ambayo imepelekea matokeo duni katika mitihani ya kitaifa.
Aidha Lonyangapuo amependekeza kuajiriwa walimu angalau 200 kila mwaka kwa shule za kaunti hii ili kuimarisha viwango vya elimu.
Wakati uo huo Lonyangapuo amependekeza kupandishwa hadhi chuo cha kisii bewa la keringet hadi kuwa chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha Kapenguria pamoja na kuzifanya shule za msingi maeneo ya mashinani kaunti hii kuwa za mabweni za gharama ya chini.