LONYANGAPUO ASHUTUMIWA KWA KAULI YAKE KUHUSU REKODI YAKE YA MAENDELEO POKOT MAGHARIBI.
Hisia mseto zimeendelea kuibuliwa na wakazi wa kaunti hii ya pokot magharibi kuhusu kauli za gavana John Lonyangapuo katika vyombo vya habari kuhusu utendakazi wake katika kipindi ambacho amekuwa mamlakani.
Wakiongozwa na Nelly Pusha, wakazi wa eneo la Kacheliba wamemsuta gavana Lonyangapuo kwa kudai kuwepo dawa za kutosha katika hospitali za kaunti hii ikiwemo ile ya kacheliba, wakisema kuwa wanapitia wakati mgumu kutafuta huduma za matibabu kufuatia uhaba wa dawa katika hospitali hiyo.
Wamewataka wakazi kutokubali kutumika na wanasiasa kuwapa sifa za bure kwa manufaa yao ya binafsi huku mwananchi akiendelea kuteseka kwa kukosa huduma muhimu za kimsingi.
Aidha wamemsuta gavana Lonyangapyuo kwa kutumia muda wake mwingi kulaumu uongozi wa mtangulizi wake badala ya kuwaelezea wananchi kile ambacho ametekeleza katika kipindi chake ambacho ameongoza kaunti hii.