LONYANGAPUO APONGEZA WAKAZI POKOT MAGHARIBI KWA USHIRIKIANO.


Gavana wa kaunti hii ya Pokot magharibi John Lonyangapuo amewapongeza wakazi wa kaunti hii kwa ushirikiano ambao wametoa kwa serikali yake katika kipindi ambacho amekuwa mamlakani.
Lonyangapuo amesema kuwa ni ushirikiano huo ndio umefanikisha maendeleo mengi ambayo ametekeleza katika muhula wake wa kwanza ikiwemo kufadhili pakubwa swala elimu kupitia basari, akitumia fursa hiyo kutangaza kuongezwa fedha zinazotengewa basari hadi shilingi alfu 20 kwa kila mwanafunzi.
Aidha Lonyangapuo amesema kuwa serikali yake imetenga kima cha shilingi milioni 60 kufadhili masomo kwa wanafunzi wawili kutoka kila wadi kaunti hii kuendeleza masomo katika mataifa ya nje.
Wakati uo huo Lonyangapuo ametoa wito kwa wawekezaji zaidi kujitokeza na kuwekeza katika kaunti hii ya Pokot magharibi ili kutoa nafasi za ajira kwa wenyeji.